pmbet

Jenerali Yaroslav wa Urusi auawa kwa mlipuko bomu

Eric Buyanza

April 25, 2025
Share :

Jenerali wa Urusi Yaroslav Moskalik ameuawa katika mlipuko wa bomu lililotegwa ndani ya gari huko Moscow. 

Kamati ya Uchunguzi ya Urusi - mamlaka kuu ya uchunguzi ya nchini humo imethibitisha hilo.

Akizungumzia mauaji hayo, msemaji wa Kamati ya Uchunguzi ya Urusi, Svetlana Petrenko, anasema: β€œGari la Volkswagen lililipuka baada ya kilipuzi kilichokuwa kimejazwa mipira kulipuka.”

Hii sio mara ya kwanza kwa wanajeshi wa Urusi kushambuliwa tangu kuanza kwa vita lakini mauaji yaliyokusudiwa huko Moscow ni nadra.

Mnamo Februari mwaka huu, Armen Sargsyan, kiongozi wa kikundi cha waasi wanaoungwa mkono Urusi mashariki mwa Ukraine, alikufa hospitalini baada ya mlipuko kutokea katika ukumbi wa kuingilia wa jengo la makazi kaskazini-magharibi mwa Moscow.

Hakuna aliyedai kuhusika na shambulio hilo.

Mnamo mwezi Desemba mwaka jana huduma ya usalama ya Ukrainia ilikubali kuwa ndiyo iliyosababisha mauaji ya jenerali wa ngazi ya juu nje ya jengo la makazi katika mji mkuu.

Luteni Jenerali Igor Kirillov, mkuu wa Kikosi cha Ulinzi cha Mionzi, Biolojia na Kemikali, aliuawa wakati kifaa kilichofichwa kwenye skuta kilipolipuliwa kwa mbali.

BBC

 

pmbet
pmbet

Leagues standings

Tanzania Premier League
pmbet
pmbet