pmbet

Jenereta la Hospitali halijatumika mwaka mzima kisa lita 15 za mafuta

Eric Buyanza

May 22, 2024
Share :

Jenereta lililotolewa na Wizara ya Afya kwa Hospitali ya Wilaya ya Busega mkoani Simiyu kwa zaidi ya mwaka mmoja halijatumika kutokana na kukosa kilo tano za chumvi, makopo mawili ya mkaa na lita 15 za dizeli. 

Hali hiyo imesababisha kukwama kwa shughuli za kitabibu hospitalini hapo hususani  umeme unapokatika, hivyo kuwalazimu kusubiri urejee.
Suala hilo liliibuliwa jana wakati wa ziara ya kushtukiza hospitalini hapo, iliyofanywa na Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Dk. Yahaya Newanda, hivyo kutoa siku tano lianze kufanya kazi mara moja.

Dk. Nawanda aliwataka Mkuu wa Wilaya hiyo, Faidha Salim na Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri hiyo, Michael Kachoma, kuhakikisha genereta hilo linaanza kazi haraka iwezekanavyo.

Mkuu huyo wa mkoa alishangazwa na uongozi wa hospitali hiyo kushindwa kugharamia vitu hivyo ambavyo havina gharama kubwa huku vitu vingine vilivyohitajika kufanikisha hatua hiyo vikitajwa kuwa ni pamoja na nyaya mbalimbali ambazo awali wataalamu walidai zinagharimu zaidi ya Sh. milioni 20.

“Taarifa nilizo nazo ni kuwa awali wataalamu walileta bajeti ya zaidi ya Sh. milioni 20. Baadaye  ikapungua hadi Sh. milioni 18. Alipokuja mkurugenzi mpya ikapungua tena hadi Sh. milioni nne lakini taarifa zilizopo inaweza kupungua hadi laki nne,” alisema.

Dk. Nawanda alisema Wizara ya Afya ilitoa jenereta hilo kwa ajili ya kusaidia huduma za upasuaji kwa wajawazito, watoto na watu wengine pindi umeme unapokatika.
“Ikifika hiyo tarehe 25 mwezi huu kabla halijaanza kufanya kazi, mkuu wa wilaya na mkurugenzi mtakuwa hamtoshi hapa. 
Haiwezekani mwaka mzima chumvi kilo tano, mkaa makopo mawili na lita 15 za dizeli mnashindwa,” alisisitiza Dk. Nawanda.

Baada ya maagizo hayo, Kachoma alimhakikishia mkuu huyo wa mkoa kuwa ifikapo tarehe iliyotolewa litakuwa tayari limeaanza kufanya kazi ili kukabiliana na adha ya utoaji huduma pindi umeme unapokatika.
NIPASHE

pmbet
pmbet

Leagues standings

Tanzania Premier League
pmbet
pmbet