Jengo la TRA Kariakoo lawaka moto
Sisti Herman
January 30, 2025
Share :

Moto ambao bado chanzo chake hakijafahamika, umewaka katika Ofisi za Mamlaka ya Mapato (TRA) zilizopo Mtaa wa Kipata, Kariakoo Jijini Dar es salaam ambapo tayari Kikosi cha Zimamoto na Uokoaji kipo kwenye eneo la tukio kuendelea na jitihada za kuuzima moto huo.
Mwandishi wa PMTV Tanzania kutoka Mtaa wa Kipata ambaye yupo eneo la tukio, amesema hadi wakati huu habari hii inapokwenda hewani, tayari ghorofa ya tano imeshateketea kwa moto.
Endelea kuwa karibu na kurasa za PMTV Tanzania kupata habari kamili kutoka eneo la tukio.





