Jeraha la kichwa kumuweka Valverde nje siku 10 hadi 14.
Joyce Shedrack
May 8, 2026
Share :
Klabu ya Real Madrid imetoa taarifa rasmi ya kitabibu kuhusu mchezaji wao Federico Valverde aliyeumia leo mazoezini baada ya kuanguka na kugonga kichwa kwenye meza kutokana na ugomvi wake na Aurelien Tchouameni.
“Baada ya vipimo vilivyofanywa leo na Idara ya Madaktari ya Real Madrid kwa mchezaji wetu Federico Valverde, amegundulika kuwa na jeraha la kichwa (craneoencephalic trauma)”.
“Valverde kwa sasa yuko nyumbani kwake akiwa katika hali nzuri, na atalazimika kupumzika kwa muda wa siku 10 hadi 14, kulingana na taratibu za kitabibu zinazotumika kwa aina hiyo ya jeraha”. Imesema taarifa ya Real Madrid.





