Jeraha lamsababisha Tyla kuhairisha ziara ya dunia
Eric Buyanza
March 8, 2024
Share :
Jeraha linalomsumbua nyota wa muziki wa Afrika Kusini ambaye pia ni mshindi wa tuzo za Grammy, Tyla, limesababisha kusitishwa kwa ziara yake ya kwanza ya dunia iliyokuwa ikisubiriwa kwa hamu na mashabiki zake.
Tyla amesitisha ziara hiyo ikiwa ni wiki mbili kabla ya kuanza, ambapo Machi 21 alitakiwa kuwa ndani ya jiji la Oslo nchini Norway.
Hata hivyo hakueleza mahali jeraha hilo lilipo wala sababu ya kupatikana kwa jeraha hilo...zaidi ya kusema ameshawasiliana na madaktari wake lakini bado anaona maumivu ni makali na hivyo kuendelea kwa tamasha kungeweza kuhatarisha afya na usalama wake.