pmbet

Jeshi la Israel lamuua Kamanda wa Hezbollah, Ali Jaafar Maatuk

Eric Buyanza

July 19, 2024
Share :

Kamanda wa jeshi katika kikosi maalum cha Hezbollah cha Radwan aliuawa katika shambulio la Israel kusini mwa Lebanon, jeshi la Israel na vyanzo viwili vya usalama vilisema jana Alhamisi.

Jeshi la Israel lilisema lilimuaa kamanda wa operesheni za kikosi cha Radwan likimtambulisha kama Jaafar Maatuk, pamoja na kamada mwingine anayehusika na operesheni za kikosi cha Radwan katika jimbo la Hajir.

Limesema wapiganaji zaidi wa kikosi cha Radwan waliuawa katika shambulio hilo.

Kiongozi wa Hezbollah Sayyed Hassan Nasrallah alionya katika hotuba siku ya Jumatano kwamba kundi lake litapanua wigo wa mashambulizi yake nchini Israel ikiwa Israel itashambulia raia zaidi.

Mapema Alhamisi, Hamas ilisema mmoja wa makamanda wake aliuawa katika shambulio la Israel eneo la Bekaa magharibi mwa Lebanon na kamanda wa Hezbollah aliuawa katika shambulio la Israel katika mji wa kusini wa Jbal el Botm.
VOA

pmbet
pmbet

Leagues standings

Tanzania Premier League
pmbet
pmbet