pmbet

Jeshi la Marekani sasa kutumia ChatGPT

Sisti Herman

September 1, 2026
Share :

 

Idara ya Ulinzi ya Marekani (Pentagon) imepiga hatua kubwa katika matumizi ya teknolojia ya akili mbandia (AI) baada ya kufungua mfumo maalum wa zana za ChatGPT na Grok kwa wafanyakazi wake wapatao milioni tatu.

Hatua hiyo inawawezesha wanajeshi pamoja me wafanyakazi wa kiraia ndani ya idara hiyo kuanza kutumia mifumo hiyo iliyoboreshwa maalum kwa ajili ya kukidhi viwango na mahitaji ya kiusalama ya jeshi la Marekani. Zana hizo zimeundwa kusaidia katika kurahisisha uchambuzi wa taarifa, usimamizi wa shughuli za kilojistiki, pamoja na kuongeza ufanisi wa utendaji kazi wa kila siku jeshini.

Uamuzi huu unatajwa kuwa moja ya hatua kubwa zaidi kuwahi kuchukuliwa na taasisi ya kiserikali duniani katika kujumuisha teknolojia ya kisasa ya chatbots katika shughuli zake za kila siku. Idara hiyo imesisitiza kuwa mifumo hiyo imewekewa ulinzi mkali wa kimitandao ili kuhakikisha usalama wa taarifa nyeti za kiulinzi unalindwa kikamilifu.

pmbet
pmbet

Leagues standings

Tanzania Premier League
pmbet
pmbet