Jeshi la polisi halihusiki na matukio ya utekaji - IGP Wambura
Eric Buyanza
July 16, 2024
Share :
Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini IGP Camillus Wambura amesema Jeshi la Polisi halihusiki na matukio yanayodaiwa kuwa ni ya utekaji kwani jukumu la msingi na la kikatiba la Jeshi hilo ni kuhakikisha linalinda usalama wa raia na mali zao.
IGP Wambura ameyasema hayo wakati akiwa mkoani Simiyu akiendelea na ziara yake ya kuzungumza na maofisa, wakaguzi na askari wa vyeo mbalimbali.