Jeshi la Polisi lamsaka mwanamke aliyemnywesha mtoto Pombe.
Joyce Shedrack
September 6, 2025
Share :
Jeshi la Polisi limesema linamsaka mwanamke aliyeonekana kwenye picha mjongeo inayosambaa katika mitandao ya kijamii akimhamasisha na kumnywesha pombe mtoto.
Taarifa iliyotolewa na Jeshi la Polisi imesema tukio hilo ni ukatili kwa mtoto na kinyume na sheria za nchi.
"Ufuatiliaji wa kina umeshaanza kama tukio hili limetokea ndani ya nchi yetu ili kuweza kumpata huyu aliyekuwa anafanya kitendo hicho kama inavyoonekana kwenye picha mjongeo hiyo," imeeleza.
Imeongeza kuwa "Tunamtaka mwanamke huyu akiona taarifa hii ajisalimishe mwenyewe katika kituo chochote cha Polisi."