Jeshi la Syria lazidiwa, laukimbia mji wa Aleppo
Eric Buyanza
November 30, 2024
Share :
Jeshi la Syria limesema idadi kubwa ya wanajeshi wake wameuwawa kufuatia shambulizi lililofanywa kaskazini magharibi mwa Syria na waasi wa Hayaz Tahrir al-Sham.
Jeshi hilo pia lilisema waasi walifanikiwa kuingia sehemu kubwa ya mji wa Aleppo hatua iliyolilazimu jeshi kuukimbia mji huo.
Taarifa hiyo ya jeshi la Syria ndiyo tamko la kwanza la jeshi hilo kukiri hadharani kwamba wanamgambo wanaoongozwa na waasi wa Hayaz Tahrir al-Sham, wameingia katika mji wa Aleppo uliokuwa chini ya serikali.