pmbet

Jeshi la Uganda lamkamata 'Fundi wa mabomu', Anywari Al-Iraq

Eric Buyanza

May 21, 2024
Share :

Jeshi la Uganda limethibitisha kumkamata kamanda wa kundi la waasi la ADF linaloshirikiana na kundi linalojiita  dola ya kiislamu, ambaye ni mtaalamu wa kutengeneza mabomu yanayotumiwa na kundi hilo kufanya mauaji. 

Kamanda huyo Anywari Al-Iraq ambaye ni raia wa Uganda, alikamatwa Mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, yalipo maskani ya kundi la hilo. 

Katika operesheni ya kumsaka watu tisa wakiwemo watoto waliokolewa kutoka katika eneo hilo lililopo mkoani Ituri Mashariki mwa DRC, huku bidhaa mbalimbali za kutengenezea mabomu zikikamatwa.

Kundi hilo la waasi wa ADF lilianza harakati zake nchini Uganda lakini limekuwa na ngome yake nchini Congo tangu miaka ya 90. 

Lilitangaza  kushirikiana na kundi linalojiita  dola la kiislamu mwaka 2019 na linatuhumiwa kufanya mauaji ya mamia ya wanavijiji katika mashambulizi ya mara kwa mara katika miaka ya hivi karibuni.

pmbet
pmbet

Leagues standings

Tanzania Premier League
pmbet
pmbet