JE,WAJUA: Korea kusini kuna sehemu za kutelekeza watoto
Eric Buyanza
February 24, 2024
Share :
JE, WAJUA
Katika hali ya kushangaza, kwenye mji wa Seoul huko Korea Kusini kwenye maeneo mbalimbali jijini humo kuna masanduku maalum (Baby Box) kwa ajili ya kutelekeza watoto...ambapo wazazi wanaweza kumtoa/kumtelekeza mtoto wao bila kujulikana.
Kama humtaki mtoto, badala ya kumtupa mtaani au kumuacha sehemu isiyo sahihi basi unafika kwenye visanduku hivyo unamuweka na kisha unapotea zako.
Masanduku ya kutelekeza watoto huko Seoul hufanya kazi masaa 24, siku saba kwa wiki.