JE,WAJUA: Simu ya kwanza ya mkononi ilikuwa na Kilo 1, ilivumbuliwa 1973
Eric Buyanza
March 14, 2024
Share :
Aprili 3, Mwaka 1973 Mhandisi wa kampuni ya Motorola, Martin Cooper alisimama kando ya barabara ya Sixth Avenue huko mjini Manhattan nchini Marekani, mkononi akiwa ameshika kifaa chenye ukubwa wa (kitofali kidogo).
Kifaa hicho si kitu kingine, bali ilikuwa ni simu ya kwanza ya mkononi aina ya Motorola DynaTAC 8000X iliyovumbuliwa na yeye mwenyewe.
Miaka 10 baadae Septemba 21 mwaka 1983, simu hiyo ilipata kibali cha serikali cha kuingizwa sokoni rasmi kama simu ya kwanza ya mkononi.
Simu hiyo ilikuwa na uzito wa kilo moja.