pmbet

Jiji la Nairobi laongoza Kenya kwa maambukizi ya Kaswende

Eric Buyanza

June 20, 2026
Share :

Idadi ya Wakenya wanaojitokeza kupimwa ugonjwa wa kaswende imeongezeka kwa kiasi kikubwa katika miaka ya hivi majuzi, huku wataalamu wa afya wakionya kuwa watoto wengi bado wanazaliwa na maambukizi hayo kwa sababu mama zao hawakupimwa wala kutibiwa wakati wa ujauzito.
 

Takwimu mpya kutoka Baraza la Kitaifa la Kudhibiti Magonjwa ya Zinaa (NSDCC), zinaonyesha kuwa watu wengi zaidi sasa wanatafuta huduma za kupimwa kaswende katika vituo vya afya kote nchini.

 

Visa vingi vimeripotiwa katika miji mikubwa, maeneo yenye shughuli nyingi za usafiri na vijiji vya mbali.Mwaka 2020, wahudumu wa afya walipima watu1.29 milioni.

 

Kufikia mwaka 2025, idadi hiyo ilikuwa imeongezeka hadi watu 1.42 milioni.

 

Kadri watu wengi walivyoendelea kupimwa, ilibainika kuwa ugonjwa huo ulikuwa tayari umeenea katika jamii lakini visa vingi havikuwa vimegunduliwa.

 

Licha ya ongezeko la vipimo, idadi ya waliopatikana na maambukizi imepungua. Mwaka 2020, karibu Wakenya 16,000 walipatikana na kaswende.
 

Kufikia mwaka 2025, idadi hiyo ilishuka hadi zaidi ya watu 9,000, sawa na kupungua kwa zaidi ya asilimia 40.Hata hivyo, kaunti 15 zilirekodi visa vya juu au vinavyoendelea kuongezeka.
 

Wataalamu wanasema hali hiyo inachangiwa na ongezeko la uhamaji wa watu mijini, mifumo dhaifu ya ufuatiliaji wa magonjwa na ukosefu wa vifaa vya kupimia na kutibu ugonjwa huo.
 

Kaunti ya Nairobi iliongoza kwa visa vingi zaidi nchini. Mwaka 2023, visa 961 vilirekodiwa huku mwaka 2025 idadi hiyo ikiongezeka hadi 1,068 kati ya watu 161,020 waliopimwa.
 

Ripoti ya NSDCC inaeleza kuwa Nairobi ni kitovu kikubwa cha usafiri na biashara ambapo maelfu ya watu huingia na kutoka kila siku, jambo linalorahisisha kusambaa kwa maambukizi.

 

Source: TaifaLeo

pmbet
pmbet

Leagues standings

Tanzania Premier League
pmbet
pmbet