pmbet

Jiji litapumua angalau, Simba na Yanga wahamia mikoani

Sisti Herman

February 1, 2024
Share :

Klabu za Simba na Yanga siku ya leo zimekwea pipa kuelekea mikoani kwaajili michezo yao ya ligi kuu Tanzania bara itakayoendelea mwishoni mwa juma hili kwenye mikoa mbalimbali huku kila timu ikicheza michezo miwili ugenini kabla ya kurejea kwenye viwanja vyao vya nyumbani jiji Dar es salaam.

 

Yanga siku yakesho ijumaa watakuwa wageni wa Kagera Sugar huko mkoani Kagera kwenye uwanja wa kaitaba mjini Bukoba huku watani zao wakiwa wegeni wa Mashujaa FC ya mkoani Kigoma kwenye uwanja wa Lake Tanganyika mjini Kigoma siku ya jumamosi.

 

Baada ya ichezo hiyo Simba na Yanga wataendelea na ziara ya mikoani, Simba watasogea mkoani Tabora kuvaana na Tabora United huku Yanga wakisafiri maili nyingi hadi nyanda za juu kusini kuwafuata Tanzania Prison.

pmbet
pmbet

Leagues standings

Tanzania Premier League
pmbet
pmbet