Jimbo la Oklahoma laamuru shule zote za Umma kufundisha somo la Biblia
Eric Buyanza
June 28, 2024
Share :
Jimbo la Oklahoma nchini Marekani limeamuru shule zote za umma kuanza kufundisha somo la Biblia.
Agizo hilo limetolewa na msimamizi wa jimbo la Republican Ryan Walters aliyesema agizo hilo ni la lazima na linatakiwa 'Kuzingatiwa kikamilifu'.
Sheria hiyo itatekelezwa kwa wanafunzi wote wa shule za umma walio na umri wa kuanzia miaka 11 mpaka 18.
Hili limekuja wiki moja baada ya Gavana wa Louisiana kutia saini sheria inayoagiza shule zote za umma katika jimbo hilo kuonyesha Amri Kumi za Mungu kwenye kila darasa la shule za umma.