pmbet

Jimbo lenye utajiri mkubwa wa madini drc lasimamisha uchimbaji

Eric Buyanza

July 20, 2024
Share :

Mamlaka katika moja ya jimbo moja lenye utajiri mkubwa wa madini mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo, imetangaza kusimamishwa kwa shughuli zote za uchimbaji madini ili "kurejesha utaratibu" katika sekta hiyo. 

Afisa Habari wa jimbo hilo la Kivu ya Kusini Danny Bashige, amesema Gavana wa jimbo hilo Jean-Jacques Purusi "anataka kudhibiti uchimbaji holela ya madini katika eneo hilo." 

Pasipo kutoa ufafanuziwa kina taarifa ya Gavama huyo inasema "shughuli za uchimbaji madini zimesitishwa hadi itakapotangazwa tena kwa sababu ya "usumbufu unaosababishwa na waendeshaji migodi.” Sababu nyingine sio tu kuyalinda maisha ya watu, lakini pia ufuatiliaji wa uzalishaji wa madini katika maeneo hayo. 

DW imeripoti kuwa kutokana na taarifa hiyo makampuni ya uchimbaji madini, wafanyabiashara na washirika wengine wamepewa masaa 72 kuondoka katika maeneo ya machimbo.

pmbet
pmbet

Leagues standings

Tanzania Premier League
pmbet
pmbet