pmbet

Jina 'Nature' nilijipa kwasababu ya uhalisi wa maisha yangu

Eric Buyanza

October 16, 2025
Share :

Jina lake halisi ni Juma Kassim, lakini mkongwe huyu kunako muziki wa Bongo fleva amekuwa akifahamika zaidi kwa jina la 'Sir Nature', katika mahojiano na Mwanaspoti hivi karibuni ameelezea chanzo halisi cha jina hilo.

Kwa mujibu wa mkongwe huyu, jina 'Sir Nature' alijipa mwenyewe akiamini linamfaa kutokana na aina ya maisha anayopenda kuishi kuwa halisi na si kufeki kama baadhi ya wasanii na watu maarufu wanavyopenda kufanya.

"Nature sijapewa na raia, bali nilisoma nikaelewa lina maana ya 'halisi' na mimi maisha yangu ni halisi. Hivyo nikaona linaendana na nilivyo" anasema.

"Jina la Sir nilijipa mimi mwenyewe pia baada ya kusoma mambo ya skauti ambapo niliona mwanzilishi alikuwa anaitwa Sir Robert Stephanson Symith Baden Powell ndipo na mimi nikajiita Sir."

pmbet
pmbet

Leagues standings

Tanzania Premier League
pmbet
pmbet