pmbet

Jini limetoka wanaoumia ni mtaa wa pili...!FT' Namungo 0-2 Yanga.

Joyce Shedrack

November 30, 2024
Share :

Baada ya kupoteza michezo miwili mfululizo ya ligi kuu klabu ya Yanga imeibuka na ushindi wa mabao mawili sifuri dhidi ya Namungo kwenye uwanja wa Majaliwa Ruangwa Mkoani Lindi.

Magoli ya Yanga yamefungwa na Kennedy Musonda dakika ya 50 ya mchezo na Pacome Zouzoua dakika ya 67 ya mchezo.

Yanga wamefikisha alama 27 kwenye msimamo wa Ligi Kuu sawa na Azam FC ambaye yupo mbele kwa michezo miwili zaidi.

Klabu ya Simba ndio vinara wa ligi wakiwa wamekusanya alama 28 katika michezo 11.

pmbet
pmbet

Leagues standings

Tanzania Premier League
pmbet
pmbet