Jinsi 'Fegi' ilivyowakutanisha Baba na Mama yake Drake!
Eric Buyanza
March 1, 2024
Share :
Dennis Graham ambaye pia alikuwa mwanamuziki (mpiga drums) anasema alikutana na mama yake Drake (Sandi) kwa mara kwanza alipokuwa kwenye show nchini Canada.
“Nakumbuka nilikuwa ukumbini kwenye show nikiwa na kiu ya fegi (sigara), nikamuuliza mhudumu wapi naweza kupata sigara?....kwa pembeni kidogo kulikuwa na mwanamke anayevuta fegi akaniangalia na kuninyooshoea pakti la sigara akaniambia....unaweza kuchukua kwangu.....na huo ndio uliokuwa mwanzo wetu" anasimulia Dennis Graham.
Dennis baadae alihamia Toronto na kumuoa Sandi Juni mwaka 1985, na oktoba ya mwaka unaofuata mungu akawajaalia mtoto kiume waliyempa jina Aubrey Drake Graham.
Hata hivyo ndoa ya wawili hao iliishia mwaka 1991, na Sandi (mama yake Drake) akapewa haki zote za kulea na kumtunza mtoto wake, kitendo kilichomfanya Drake kumuona baba yake mara chache sana kwa mwaka