pmbet

João Pedro ataweza kuvunja "Gundu" la jezi namba 9 ya Chelsea?

Eric Buyanza

August 21, 2026
Share :

Chelsea wamethibitisha rasmi kuwa mshambuliaji João Pedro ndiye atakayevaa jezi namba 9 msimu mpya wa 2026-27, akichukua nafasi ya Liam Delap ambaye sasa amepewa jezi namba 12.

 

Mashabiki na wachambuzi wengi wanataja jezi namba 9 ya Chelsea kama namba yenye "gundu au mkosi".

Mchezaji huyo raia wa Brazil amekubali kikamilifu shinikizo linaloambatana na jezi hiyo, akisisitiza kuwa "laana ya namba 9" ambayo imekuwa na sifa mbaya na klabu hiyo,  haimtishi; badala yake, inampa motisha.

 

"Laana ya namba 9 hainitishi, inanipa motisha. Niliiomba namba hii kwa sababu nataka jukumu la kuwa mshambuliaji tegemeo wa Chelsea. Namba yenyewe haileti bahati mbaya, bali mchezaji ndiye anayefanya hivyo. Nipo hapa kuivunja laana hiyo na kuifanya namba 9 kuwa ya kipekee tena."

 

Wachezaji wakubwa kama Fernando Torres, Alvaro Morata, na Romelu Lukaku walishindwa kung'ar wakiwa na namba hiyo.

 

Je, João Pedro ataweza hatimaye kuivunja laana hiyo?

pmbet
pmbet

Leagues standings

Tanzania Premier League
pmbet
pmbet