pmbet

"Job hajaitwa Stars kwasababu ya utovu wa nidhamu" - Jemedari

Sisti Herman

March 14, 2024
Share :

Mchambuzi maarufu wa soka nchini Jemedari Said amebainisha kuhusiana na uchunguzi alioufanya wa sababu za beki wa Yanga Dickson Job kutoitwa kwenye kikosi cha timu ya Taifa Tanzania kinachojiandaa kucheza FIFA Series huku akisema wazi kuwa Job kutoitwa kumesababishwa na kupishana kauli na kaimu kocha mkuu Hemed Suleiman "Morocco".

 

Hizi ni nukuu za Jemedari alizochapisha kupitia kurasa zake za mitandao ya kijamii

 

“Sababu kubwa na ya msingi ya kuachwa Dick Job ni utovu wa nidhamu na kukosa uzalendo kwa kitendo cha kukataa kucheza mechi dhidi ya Congo DR ambayo ilikuwa muhimu kwa Taifa Stars mchezo uliochezwa pale Korogho Ivory Coast.

“Kocha Morocco aliyekuwa anakaimu ukocha wa Stars baada ya Amrouche kusimamishwa na CAF, alimpanga Job nafasi ya beki wa pembeni kulia (namba 2), kisha akaita kikosi kufanya nacho kikao kazi kabla ya mechi na kuelekeza mbinu za kuikabili DRC kwenye mchezo huo, baada ya kumaliza ndipo Job alinyoosha kidole akasema yeye hayuko tayari kucheza namba 2.

“Ikabidi kocha ambadilishe na nafasi yake kupewa Lusajo Mwaikenda wa Azam ambaye alipambania Taifa mpaka mwisho. Inaelezwa nahodha wa Stars MBWANA Samatta aliongea na kocha kwamba angeongea na Job ili acheze lakini kocha akamwambia muache usimlazimishe. Mechi iliisha kwa sare ya 0-0.”

 

Alichagiza hivyo Jemedari kuhusiana na mjadala mkubwa kwenye vyombo mbalimbali vya habari.

pmbet
pmbet

Leagues standings

Tanzania Premier League
pmbet
pmbet