Jobe Bellingham afanya maamuzi ya kufata nyayo za kaka yake.
Joyce Shedrack
June 3, 2025
Share :
Mchezaji wa Timu ya Taifa ya Uingereza chini ya umri wa miaka 21 na klabu ya Sunderland iliyokuwa ikishiriki ligi daraja la kwanza ‘Championship’ Nchini Uingereza Jobe Bellingham anatarajia kujiunga na klabu ya Borussia Dortmund ya Ujerumani.
:max_bytes(150000):strip_icc():focal(1020x506:1022x508)/jude-bellingham-brother-jobe-bellingham-1-6446bd5df4594018b6f02bde0b21e93a.jpg)
Kiungo huyo mwenye umri wa miaka 19 ambaye ni ndugu wa damu na mchezaji wa Real Madrid Jude Bellingham amechagua kujiunga na klabu ya zamani aliyowahi kuitumikia kaka yake inayoshiriki ligi kuu Nchini Ujerumani.
Nyota huyo aliyejiunga na Sunderland mwaka 2024 mkataba wake ndani ya klabu hiyo itakayoshiriki ligi kuu Uingereza msimu ujao unatarajia kutamatika msimu wa mwaka 2027/28 .
Jobe msimu uliopita ameisaidia klabu yake kupanda ligi kuu ya Uingereza baada ya kucheza mechi 43 akifunga magoli 4 na kutoa pasi 3 za magoli.





