pmbet

John aenda jela miaka 15, kwa kutaka kumbaka Bibi kizee wa miaka 80

Eric Buyanza

June 21, 2024
Share :


Mahakama ya hakimu Mkazi Wilaya ya Lindi Juni 21, 2024 imemuhukumu kwenda jela miaka 15 John Swaki Fokasi (33) kwa kosa la kujaribu kumbaka bibi wa miaka 80.
 

Mtuhumiwa huyo alitenda kosa hilo Aprili 03, 2024 huko Tulieni Mashambani majira ya saa sita usiku alipomvamia bibi huyo kwenye nyumba aliyokuwa amejihifadhi.
 

Alipoanza purukushani za kutaka kumuingilia kinguvu kimapenzi bila ridhaa yake kizee huyo alijiokoa kwa kumkata panga sehemu ya kichwani na mkononi ndipo mtuhumiwa huyo akakimbia kusiko julikana mpaka alipokamatwa siku iliyofuta na kufikishwa mahakamani.
 

Hukumu hiyo ya kesi namba 10546/2024 imetolewa na hakimu mkazi wa mahakama hiyo Mhe. Deliphina Kimati ili iwe fundisho na kwa wengine wenye tabia kama hizo.

pmbet
pmbet

Leagues standings

Tanzania Premier League
pmbet
pmbet