John Bocco arejea rasmi Simba kama Kocha
Sisti Herman
December 26, 2025
Share :

Aliyekuwa nahodha wa Simba SC na Mfungaji bora wa muda wote wa Ligi Kuu Tanzania John Bocco amerejea Simba Sports Club kama Kocha Mkuu wa timu za vijana zote akitokea JKT Tanzania baada ya kumaliza mkataba wake kama mchezaji.
John Bocco ambaye anamiliki leseni B ya shirikisho la soka Afrika CAF, amepewa programu nzima ya maendeleo ya vijana ndani ya Simba Sports Club.





