John Stones kuwaaga mashabiki Etihad mwishoni mwa msimu
Eric Buyanza
April 29, 2026
Share :

Mlinzi wa kati wa Manchester City John Stones anatarajiwa kuondoka mwishoni mwa msimu huu baada ya kuitumikia klabu hiyo kwa muongo mmoja.
Stones alikuwa mmoja wa wachezaji wa kwanza kusajiliwa na Pep Guardiola mwaka 2016 na amecheza takriban mechi 300 akiwa na City, na kuisaidia kushinda mataji 19 makubwa, yakiwemo mataji sita ya Ligi Kuu na Ligi ya Mabingwa 2023.
Beki anakuwa mchezaji wa pili wa muda mrefu kutangaza kuondoka baada ya Bernardo Silva.
“Pamekuwa kama nyumbani kwangu kwa miaka 10 iliyopita, na patakuwa nyumbani kwangu kwa maisha yangu yote," Stones aliandika kwenye ukurasa wake wa Instagram.





