Jokate achaguliwa kuwa katibu Mkuu UVCCM
Sisti Herman
April 3, 2024
Share :
Halmashauri Kuu ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) iliyokutana leo April 03, 2024 Jijini Dar es salaam, katika kikao chake maalum, chini ya Mwenyekiti wa CCM na Rais wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan, pamoja na masuala mengine imemchagua Jokate Urban Mwegelo kuwa Katibu Mkuu wa Umoja wa Vijana wa CCM, akichukua nafasi ya Fakii Raphael Lulandala ambaye ameteuliwa kuwa Mkuu wa Wilaya ya Simanjiro.