Jokate; Rais Samia anastahili tuzo ya Nobel
Sisti Herman
May 27, 2024
Share :
Kupitia makala maalum aliyoiandika kwenye Gazeti la Brussels Morning la nchini Ubelgiji, akishirikiana na mwandishi mwenza Seleman Kitenge, Katibu Mkuu wa Umoja wa vijana wa Chama Cha Mapinduzi (UVCCM) Jokate Mwegelo amesema Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan anastahili kushinda tuzo ya heshima ya Nobel kutokana na jitihada zake katika maridhiano, Ustahimilivu, mabadiliko na kujenga upya ambazo zote zipo kwenye falsada ya 4R za Samia.
Hizi ni baadhi ya nukuu ambazo zipo kwenye makala hiyo;
"Rais Samia Suluhu Hassan, rais wa kwanza mwanamke wa Tanzania, aliingia madarakani kufuatia kifo cha Rais Dkt. John Pombe Magufuli kilichotokea Machi 2021. Uongozi wake umegubikwa na juhudi za kuponya migawanyiko ya kisiasa na kukuza demokrasia kupitia falsafa yake ya 4Rs: Maridhiano, Ustahimilivu, Mageuzi, na Kujenga Upya. Licha ya mashaka ya awali kutokana na jinsia yake, Rais Samia ametekeleza mageuzi makubwa, ikiwa ni pamoja na kuondoa marufuku ya mikutano ya kisiasa, kugeuza sera za kurudi nyuma, na kuanzisha mageuzi ya uchaguzi. Juhudi zake zimesababisha hali ya kisiasa inayojumuisha zaidi, na kutoa hoja kali ya kuzingatia kwake kwa Tuzo ya Amani ya Nobel"
"Juhudi zilizofanywa na Rais Samia kutekeleza falsafa yake ya 4Rs zinasisitiza suala la lazima kwa kuzingatia kwake kwa Tuzo ya Amani ya Nobel. Si mpigania tu misingi ya demokrasia na utawala wa sheria bali pia ni mjenga amani dhabiti ambaye amefanikiwa kupatanisha, kurekebisha na kujenga upya mazingira ya kisiasa ya Tanzania ili kujumuisha sauti za vyama vyote vya siasa, asasi za kiraia na makundi mengine ya kijamii licha ya changamoto zilizopo"
Tuzo za Nobel ni mkusanyiko wa tuzo tano tofauti zinazotolewa kwa wale ambao, katika mwaka ulihusika, wametoa manufaa makubwa zaidi na kuacha alama kubwa sana kwa jamii na Mataifa kama ilivyoanzishwa na wosia wa 1895 wa mwanakemia, mhandisi, na mwana viwanda wa Uswidi Alfred Nobel, mwaka mmoja kabla ya kifo chake.