Jol Master: Hakuna 'Comedian' anayenishinda Tanzania
Sisti Herman
June 12, 2024
Share :
Msanii maarufu wa vichekesho nchini Juma Omary Laurent 'Jol Master' kupitia ukurasa wake wa mtandao wa kijamii wa instagram ameandika kwenye Insta story yake kuwa hakuna msanii wa vichekesho 'Comedy' anayemzidi uwezo na thamani kwasasa.
"Mimi ni mchekeshaji namba moja na ghali zaidi"
"Onyesho langu maalum likitoka itawaziba wote midomo wazi"
"Naweza kuandika, naweza ku-perfom, naweza kuburudisha, mimi ni star"
"Bongo hii sijaona mkali kunishinda"
"Mnaobisha leteni 'Comedy Special' za lisaa limoja za Comedian bora, wote niwaletee yangu then tuongee Lugha moja"
Ameandika hivyo Jol Master kupitia Insta Story yake.
Je kwa upande wako unadhani nani 'Comedian' bora kwasasa nchini?