Jonathan Majors wa Avengers ndo basi tena
Sisti Herman
December 19, 2023
Share :
Kampuni za Marvel na Walt Disney zinazohusika na uzalishaji filamu zimevunja mkataba na Mwigizaji Jonathan Majors baada ya Mahakama kumkuta na hatia ya kumpiga na kumnyanyasa kimwili, Grace Jabbari, aliyekuwa mpenzi wake ambaye alimfungulia Kesi Machi 2023.
Mwigizaji huyo alijipatia umaarufu kupitia filamu za The Harder They Fall, Creed III, Loki, Lovecraft Country, Ant-Man and the Wasp: Quantumania na Devotion. Pia, alitarajiwa kuonekana katika Filamu za Avengers: The Kang Dynasty na Avengers: Secret Wars.