Jonathan Sowah na Simba ndo basi tena.
Joyce Shedrack
April 9, 2026
Share :
Taarifa zinaeleza kuwa mshambuliaji wa kimataifa wa Ghana, Jonathan Sowah ameandika barua ya kuomba kuvunja mkataba wake kwa wekundu wa Msimbazi Simba baada ya kutoridhishwa na tuhuma zilizotolewa kwake na kupelekea kusimamishwa kucheza mpira.

Sowah ambaye alijiunga na Simba dirisha kubwa la usajili akitokea Singida Black Stars ameifungia klabu hiyo magoli matatu kabla ya kusimamishwa akisubiri maamuzi ya kamati ya nidhamu ya Simba kuhusu tuhuma zinazomkabili.





