Jose Chameleone atangaza kuacha pombe baada ya kunusurika kifo.
Joyce Shedrack
April 23, 2025
Share :
Habari njema kwa mashabiki wa mkongwe wa muziki wa Uganda Jose Chameleone ni kuwa amesema ameacha kuvuta sigara na kunywa pombe.
Akizungumza na wanahabari alipowasili katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Jomo Kenyatta jijini Nairobi, msanii huyo mwenye umri wa miaka 44 alionekana kuwa mwembamba sana kwani alipokuwa marekani alipoteza kilo 13 wakati wa matibabu, lakini alikuwa ameimarika.
"Mungu amenipa nafasi nyingine," aliwaambia waandishi wa habari. "Nimezaliwa upya."
Chameleone, anayefahamika zaidi kwa vibao kama vile Kipepeo, Badilisha na wale wale, alisema uamuzi huo unafuatia kile alichoeleza kuwa ni wakati wa kujitathmini baada ya vita vya muda mrefu vya afya na wala hajakatazwa na Daktari .
Katika mahojiano ya hivi karibuni, alikiri kuwa na mapambano ya muda mrefu na matumizi ya madawa ya kulevya.