Jose Mourinho atamani kurejea Manchester United
Eric Buyanza
February 1, 2024
Share :
Jose Mourinho, ambaye majuma mawili yaliyopita alifutwa kazi na klabu ya Roma, anatamani kurejea Manchester United kama meneja wa klabu hiyo ya Old Trafford iwapo nafasi hiyo ingetokea, gazeti la Daily Mail linaripoti.
Meneja huyo wa Ureno ana matumaini ya kufanya kazi na wamiliki wapya wa United Sir Jim Ratcliffe na INEOS, ambao wanasimamia shughuli za soka tangu kununua asilimia 25 ya hisa katika klabu hiyo.
Wakati Mourinho akitafuta gia ya kurejea United, klabu hiyo haitafuti meneja mpya kwa wakati huu kwani meneja wa sasa Erik ten Hag bado ana kandarasi hadi 2025.
Mourinho alitumia takribani miaka miwili na nusu kuinoa United kabla ya kutimuliwa Desemba 2018. Aliwaongoza Mashetani Wekundu hao kushinda Ligi ya Europa, Kombe la Carabao na Ngao ya Jamii.