Jose Mourinho kupewa mkataba mpya Roma kwa masharti hayaa!
Eric Buyanza
January 10, 2024
Share :
Roma wanaripotiwa kukaribia kwenye makubaliano na Jose Mourinho kuhusu kuongezewa mkataba ambao utamfanya meneja huyo wa Ureno aendelee kusalia katika klabu hiyo.
Katika wiki za hivi karibuni, mengi yamesemwa kuhusu mkataba wa Mourinho na klabu hiyo wakati huu ambapo imesalia miezi michache tu kumalizika kwa mkataba wake.
Inaripoti kuwa Roma wameamua kuendelea kupata huduma ya 'The Special One' kwa angalau kwa mwaka mwingine na wanaharakisha makubaliano yaweze kufikiwa kabla ya mwezi Frebruari.
Taarifa za kuaminika zinasema mkataba huo huenda ukawa na masharti fulani yanayohusishwa na kufuzu kwa timu kwenye Ligi ya Mabingwa.