Joseph Kabila ameonekana Nairobi baada ya kuhukumiwa kifo
Sisti Herman
October 17, 2025
Share :
Joseph Kabila, aliyewahi kuwa Rais wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC), ameonekana jijini Nairobi siku chache baada ya kuhukumiwa kifo kwa kosa la uhaini na kuvuruga amani.
Hukumu hiyo ilitolewa na mahakama ya kijeshi ya DRC mnamo Septemba 30, bila yeye kuwepo mahakamani.
Kabila anaripotiwa kuwa nchini Kenya kwa ajili ya mikutano ya kisiasa na viongozi wa upinzani wanaopinga utawala wa Rais Félix Tshisekedi.
Uwepo wake umeibua maswali ya kidiplomasia na kisiasa katika ukanda wa Afrika ya Kati na Mashariki.
Serikali ya DRC haijatoa tamko rasmi kuhusu harakati za Kabila, huku mashirika ya haki za binadamu yakifuatilia kwa karibu maendeleo ya kesi hiyo.