pmbet

Joto la kutisha laua zaidi ya watu 5,000 Ujerumani

Eric Buyanza

July 10, 2026
Share :

Taasisi ya Afya ya Umma ya Ujerumani, Robert Koch, imesema watu wanaokadiriwa kufikia 5,120 wamefariki dunia kutokana na athari za joto kali tangu mwanzoni mwa mwaka huu wa 2026.

 

Sehemu kubwa ya vifo hivyo vilitokea mwishoni mwa mwezi Juni wakati wastani wa joto kwa wiki ulipozidi nyuzi 20 za Selsiasi. Takribani watu 4,270 waliofariki walikuwa na umri wa miaka 75 na kuendelea.
 

Wakati huo huo, huduma ya Copernicus ya Umoja wa Ulaya imesema Ulaya Magharibi imeshuhudia mwezi Juni wenye joto kali zaidi kuwahi kurekodiwa, huku nchi kadhaa zikiripoti maelfu ya vifo vya ziada vilivyohusishwa na wimbi la joto.

 

DW

pmbet
pmbet

Leagues standings

Tanzania Premier League
pmbet
pmbet