Julian Alvarez kwenye Dunia yake...! Miaka 24 makombe 16
Joyce Shedrack
July 15, 2024
Share :
Mshambuliaji wa Timu ya Taifa ya Argentina na klabu ya Man City Julian Alvarez ameingia kwenye rekodi ya wachezaji wenye umri mdogo kushinda mataji mengi na makubwa Duniani akiungana na mchezaji nguli wa Brazil Ronaldinho,Dida pamoja na Cafu.
Alvarez mwenye umri wa miaka 24 tayari ameshatwaa makombe 16 akiwa na Timu ya Taifa ya Argentina, Man City na Timu yake ya zamani River Plate akishinda mataji yote makubwa kama Kombe la Dunia mwaka 2022, Klabu Bingwa Ulaya akiwa na Man City mwaka 2023, Copa Amerika 2021 na 2024,Copa Libertadores 2018,UEFA Super Cup 2023 na Club World Cup 2023.
Makombe mengine aliyowahi kushinda mchezaji huyo ni Copa Argentina (2019), Supercopa Argentina (2019),South American U-23 Pre-Olympic Tournament (2020),Argentina Primera Division Tournament (2021),Trofeo de Campeones (2021),Finalissima (2022),Premier League (2023),FA Cup (2023)
- na Premier League (2024).
Alvarez alianza kuzitumikia timu hizo tatu kwa nyakati tofautitofauti tangu mwaka 2018 alipokuwa na River Plate na kuanza safari ya matumaini iliyompa mafanikio makubwa ndani ya muda mfupi.