pmbet

Julio abeba mikoba kuikoa Singida shimoni

Sisti Herman

March 13, 2024
Share :

Klabu ya Singida Fountain Gate FC imemtambulisha Jamhuri Kiwelu (Julio) kuwa kocha mkuu wa timu hiyo hadi mwisho wa msimu baada ya wiki iliyopita kuvunja benchi zima la ufundi lililokuwa chini ya Thabo Senong.

Singida FG imeamua kumpa kazi Julio baada ya kutoridhishwa na matokeo ya timu yao ilipokuwa chini ya Senong.

Singida FG kwa sasa inashika nafasi ya 12 kwenye msimamo wa Ligi Kuu Tanzania Bara baada ya kuvuna pointi 21, pointi 28 nyuma ya vinara wa ligi hiyo, Yanga.

Timu hiyo imebakiza mechi 10 kuamua hatima yao kama itaendelea kubaki kwenye Ligi Kuu au itaporomoka kwenda kwenye Championship msimu ujao.

Wengine walioongezwa kwenye benchi hilo la ufundi ni pamoja na aliyekuwa kocha wa muda wa timu hiyo Ngawina Ngawina ambaye kwa sasa ni kocha msaidizi na Ally Mustapha ‘Barthez’ kuwa kocha wa makipa.

pmbet
pmbet

Leagues standings

Tanzania Premier League
pmbet
pmbet