Juma aenda jela maisha kwa kumbaka mtoto wa miaka 3
Eric Buyanza
August 29, 2026
Share :

Mahakama ya Wilaya ya Pangani imemhukumu Juma Zakayo Nima, mwenye umri wa miaka 40 na mkazi wa Mtango Village, kutumikia kifungo cha maisha jela baada ya kupatikana na hatia ya kumbaka mtoto mwenye umri wa miaka 3.
Akisoma hukumu hiyo tarehe 28 Agosti 2026, Hakimu Mhe. Magwiza amesema Mahakama imeridhishwa na ushahidi uliowasilishwa na upande wa mashtaka na hivyo kujiridhisha kuwa kosa hilo limethibitishwa dhidi ya mshtakiwa.
Hakimu Mhe. Magwiza amesema hukumu hiyo imetolewa kwa kuzingatia sheria na kuhakikisha haki inatendeka, huku ikiwa ni fundisho kwa watu wengine wanaoweza kujihusisha na vitendo vya ukatili dhidi ya watoto.
Kwa mujibu wa maelezo ya kesi, mtuhumiwa alifikishwa mahakamani kwa kosa la kumbaka mtoto mwenye umri wa miaka 3, ambaye ni mwanafunzi wa Darasa la Kwanza.
Kesi hiyo yenye Namba CC No. 17946/2026 ilisikilizwa katika Mahakama ya Wilaya ya Pangani, ambapo baada ya kusikiliza ushahidi uliowasilishwa, Mahakama ilimkuta Juma Zakayo Nima na hatia.
Mahakama imemhukumu mtuhumiwa huyo kutumikia kifungo cha maisha jela.
Source: @polisi.tanzania





