pmbet

Jumba jeupe laiponza Yanga yatakiwa kulipa milioni 30

Eric Buyanza

May 11, 2026
Share :

Kamati ya Uendeshaji na Usimamizi wa Ligi ya Bodi ya Ligi Kuu Tanzania (TPLB) imeipiga faini ya kiasi cha Sh. Mil 30 klabu ya Yanga SC kwa kosa la wachezaji na maofisa wake wa ufundi kukataa kutumia chumba rasmi cha kuvalia kwenye uwanja wa Meja Jenerali Isamuhyo, Jijini Dar es Salaam.

Yanga SC ambao ndio vinara wa Ligi Kuu hawajatumia vyumba hivyo katika pambano lao na Simba SC na badala yake walitumia nyumba iliyo nje ya uwanja upande wa pili wa Barabara kinyume na matakwa ya kanuni ya 17:20 ya Ligi Kuu kuhusu Taratibu za Mchezo.

Katika kikao chake cha Mei 9, 2026 cha TPLB ilipitia mwenendo na matukio mbalimbali ya Ligi na kufanya maamuzi hayo kwa Yanga SC katika mchezo huo namba 169 na ulimalizika kwa sare ya kufungana 2-2.

Adhabu hii ni kwa mujibu wa Kanuni ya 27:7 ya Ligi Kuu kuhusu Vyombo vya Maamuzi na Yanga SC pia imepewa onyo kali kwa kosa la kuchelewa kuwasili kwenye uwanja huo baada ya kuwasili uwanjani saa 10:35 alasiri badala ya saa 10:30 alasiri jambo ambalo ni kinyume na matakwa ya Kanuni ya 17:15 ya Ligi Kuu kuhusu Taratibu za Mchezo.

pmbet
pmbet

Leagues standings

Tanzania Premier League
pmbet
pmbet