pmbet

Jurgen Klopp awavimbia Marekani.

Joyce Shedrack

July 12, 2024
Share :

Aliyekuwa Kocha Mkuu wa klabu ya Liverpool Jurgen Klopp ametupilia mbali ofa ya kuwa kocha mkuu wa timu ya taifa ya Marekani.

Shirikisho la soka la nchi hiyo lilimuhitaji Klopp kurithi mikoba ya Gregg Berhalter aliyefutwa kazi kwenye timu hiyo baada ya kutupwa nje kwenye michuano ya Copa America 2024.

Timu ya Taifa ya Marekani iliishia hatua ya makundi baada ya kumaliza nafasi ya tatu kwenye Kundi lao nyuma ya Uruguay na Panama na kushindwa kufuzu hatua ya robo fainali ya michuano hiyo.

Klopp alitangaza kujiuzulu kuwa kocha mkuu wa Liverpool kwa lengo la kuchukua mapumziko ya kufundisha soka.

pmbet
pmbet

Leagues standings

Tanzania Premier League
pmbet
pmbet