Jux amvalisha mpenzi wake pete ya pili yenye thamani ya Milioni 130.
Joyce Shedrack
February 13, 2025
Share :
Mwanamuziki wa Bongofleva Juma 'Jux' usiku wa jana alimvalisha pete mke wake raia wa Nigeria Priscila Ojo kwa mara ya pili mbele ya wazazi wake na marafiki wa karibu.
Jux amethibitisha kuwa pete aliyomvalisha mke wake ni Diamond na ina thamani ya $50,000 ambayo ni zaidi ya Milioni 130 kwa pesa za kitanzania.
Ikumbukwe,wawili hao walifunga ndoa Februari 7, 2025 iliyohudhuriwa na familia, marafiki wa karibu, pamoja na baadhi ya mastaa wa Bongo Fleva, wakiwemo Naseeb Abdul ‘Diamond Platnumz’, ambaye ni CEO wa Lebo ya WCB, na wengine wengi.