Jux na Pricsilla wapata mtoto wao wa kwanza.
Joyce Shedrack
August 25, 2025
Share :
Staa wa Bongo Fleva, Juma Mkambala maarufu 'Jux' na mke wake Priscilla wamebarikiwa kupata mtoto wao wa kwanza wakiume Agosti 24,2025 aliyezaliwa nchini Canada na kumpatia jina la Rakeem Ayomide Mkambala.
Kupitia kurasa zao za mitandao ya kijamii ya mwanamuziki huyo na mke wake Priscilla wamechapisha picha wakithibitisha ujio wa mtoto huyo wa kiume katika ndoa yao iliyofungwa miezi michache iliyopita.
Rakeem ambaye anakuwa mtoto wa kwanza kwa wawili hao ambao walifunga ndoa Februari 7, 2025, nyumbani kwa mwanamuziki huyo Mbezi, Jijini Dar es Salaam baada ya kukutana Agosti 2024 Nchini Rwanda na kuanza safari ya mapenzi iliyochipua na kuzaa matunda.