Jux na Priscilla watimiza mwaka mmoja wa ndoa yao.
Joyce Shedrack
February 7, 2026
Share :
Mwanamuziki Jux pamoja na Mke wake Hadiza leo February 7 wanasheherekea Mwaka Mmoja tangu walipofunga ndoa ya Nikkah Februari 2025 huku mtoto wao Rakeem akiwa amefikisha miezi Mitano tangu alipozaliwa september 24 2025.
Jux na Priscy walifunga ndoa miezi sita baada ya kuanza mahusiano yao huku Couple yao kwa hivi sasa ikiwa moja ya Couple maarufu na inayotajwa zaidi Afrika ikiwavutia wengi kutokana na ustaa walionao kwenye nchi zao Tanzania na Nigeria, Utamaduni wao lakini na Jamii inavyozichukulia familia hizo mbili tangu zilipokutanishwa na watoto wao.
Jux amepata mafanikio mengi tangu alipokutana na kuoana na Priscy kwa sapoti anayompatia, Ngoma zake kuwa streamed zaidi wenye charts za Kimuziki, kupata mashabiki wapya wa kazi zake ikiwemo brand yake ya African boy, Show nyingi alizofanya na kupata tuzo mbali mbali, kufanya kolabo na wasanii wa nnje jambo linalompelekea kwa hivi sasa kutizamwa kama msanii wa Kimataifa.





