pmbet

Kadi nyekundu 23 zatolewa kwenye mchezo wa derby Nchini Brazil.

Joyce Shedrack

March 9, 2026
Share :

Soka la Brazil usiku wa kuamkia leo limeshuhudia tukio la ajabu sana wakati wa fainali ya mashindano ya kikanda ya Campeonato Mineiro. 

 

Mchezo wa Dabi kali kati ya Cruzeiro na Atlético Mineiro umeingia kwenye rekodi ya kihistoria ya kadi nyekundu 23 kutolewa baada ya vurugu iliyotokea mwishoni kabisa mwa mchezo.

 

Dakika za mwisho za mchezo huo mzozo kati ya baadhi ya wachezaji ulikuwa mkubwa na kuibuka kwa mapigano yaliyohusisha karibu kila mtu aliyekuwa uwanjani.

Brazil: 23 red cards handed out during the derby between Cruzeiro and Atlético  Mineiro - Foot Africa

Ngumi, kusukumana na makabiliano ya uso kwa uso vilitumbukiza uwanja mzima katika mkanganyiko mkubwa huku wachezaji wa benchi wakikimbilia uwanjani, pamoja na makocha na wafanyakazi wa timu kujiunga kwenye vurugu, hali iliyofanya iwe vigumu kudhibiti tukio hilo kwa dakika kadhaa.

 

Kutokana na uzito wa tukio hilo, mwamuzi wa mechi alilazimika kuchukua hatua kali kulingana na ripoti rasmi ya mechi, wachezaji 23 walitolewa nje kwa kadi nyekundu, na hivyo kuweka rekodi mpya katika historia ya soka ya Brazil,kadi nyekundu 12 kwa timu ya Cruzeiro na 11 kwa Atlético Mineiro. 

 

 

 

 

 

 

 

pmbet
pmbet

Leagues standings

Tanzania Premier League
pmbet
pmbet