pmbet

Kadi Nyekundu ya Derick Mukombozi dhidi ya Simb yafutwa.

Joyce Shedrack

February 23, 2025
Share :

Kamati ya Uendeshaji na Usimamizi wa Ligi imefuta adhabu ya kadi nyekundu (Red Card) aliyooneshwa mchezaji wa Namungo Derick Mukombozi na mwamuzi wa mchezo wa Ligi Kuu kati ya Namungo dhidi ya Simba uliochezwa tarehe 19 Februari 2025.

Taarifa iliyotolewa siku ya leo na Bodi ya Ligi Kuu Tanzania (TPLB) imeeleza kuwa kamati imefikia maamuzi hayo baada ya kujiridhisha kuwa maelezo yaliyopo kwenye ripoti ya mwamuzi hayana ushahidi wa kutosha unaoendana na marejeo ya picha mjongeo kuwa Mukombozi alistahili kadi nyekundu.

 

Aidha,Mchezaji wa Namungo Daniel Amoah ametozwa faini ya shilingi laki tano kwa kosa la kuonekana akimwaga kimiminika kwenye goli jambo ambalo lilihusianishwa na vitendo vya imani za kishirikina.

 

Amoah alionekana akifanya kosa hilo wakati timu ya Simba ikijiandaa kupiga penati.

pmbet
pmbet

Leagues standings

Tanzania Premier League
pmbet
pmbet