Kagame achaguliwa tena kugombea urais wa Rwanda
Eric Buyanza
March 11, 2024
Share :
Rais Paul Kagame wa Rwanda amechaguliwa tena na chama chake cha Rwandan Patriotic Front (RPF) kuwa mgombea urais katika uchaguzi unaotarajiwa kufanyika Julai 7, 2024.
Kagame amekuwa rais tangu mwaka 2000, juzi Jumamosi alichaguliwa kwa asilimia 99.1 ya kura kulingana na taarifa ya chama hicho.
Akihutubia chama hicho baada ya kuidhinishwa kuwa mgombea, Kagame aliwashukuru wanachama kwa kuendelea kumuamini.