Kagame: Afrika inaweza kulisha dunia nzima
Sisti Herman
September 2, 2025
Share :
Rais wa Rwanda Paul Kagame amelitaka bara la Afrika kuacha kutegemea dunia katika kila kitu na kusisitiza kwamba, bara hilo linaweza kujitegemea kwa sababu lina utajiri wa rasilimamali zote.
Rais Kagame aliyasema hayo katika mkutano wa Africa Food Systems Forum jijini Dakar, Senegal, utakaoendelea hadi Septemba 5, ambao unalenga kuwaleta pamoja wadau mbalimbali ili kukuza mifumo ya kilimo endelevu na jumuishi barani Afrika.