Kagame asema hajui kama vikosi vyake viko DRC Kongo
Eric Buyanza
February 4, 2025
Share :
Rais wa Rwanda, Paul Kagame amesema hajui kama kuna vikosi vya nchi yake kwenye nchi jirani ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo.
Akijibu swali aliloulizwa kwenye mahojiano maalum na mtangazaji wa CNN, Larry Madowo Jumatatu, Februari 3, swali lililotaka kujua kama nchi yake imepeleka wanajeshi nchini Kongo Kagame alisema HAJUI.
"Sijui,".....βKuna mambo mengi sijui. Lakini ukitaka kuniuliza, kuna tatizo huko Kongo ambalo linahusu Rwanda...Na kwamba Rwanda ingefanya lolote kujilinda, Ningejibu ndio kwa asilimia 100,β na kuongeza kuwa hawezi kuwazuia watu kusema chochote wanachotaka kusema."
"Naweza kuitwa chochote, naweza kufanya nini juu ya hilo?" Aliuliza. "Lazima tufanye kile tunachopaswa kufanya ... lazima tuhakikishe tunajinusuru na dhoruba yoyote ambayo inavuma katika nchi yetu."
Takriban miili 900 imeopolewa kutoka mitaa ya Goma tangu ghasia kuzuka.