Kagame azindua kampeni za uchaguzi Rwanda
Sisti Herman
June 23, 2024
Share :
Rais wa Rwanda Mgombea katika kiti hicho kwa muhula wa nne Paul Kagame, ameanza kampeni kuelekea katika uchaguzi mkuu uliopangwa kufanyika Julai 15.
Amezindua kampeni zake katika uwanja wa mpira wa Busogo uliopo Musanze nje ya mji wa Kigali.
Rais Kagame anawania muhula wa nne akichuana na wagombea wengine wawili ambao pia wananza kampeni zao leo licha ya Kagame kupewa nafasi kubwa ya kuibuka mshindi.
Hata hivyo, Upinzani unamshutumu Rais Paul Kagame kwa kuuminya hasa kukatwa majina yao wasishiriki katika chaguzi mbali mbali hasa kiti cha Urais licha ya baadhi ya wagombea kukidhi vigezo.